Na Mwandishi wetu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amewasili jijini Addis Ababa, Ethiopia Mei 08, 2026 na kukutana na Balozi wa Tanzania nchini humo mwenye makazi Yake Ethiopia, Mheshimiwa Innocent Shio.
Katika kikao hicho, Mheshimiwa Waziri Kombo amempongeza Balozi Shio kwa namna anavyoendelea kuiwakilisha Tanzania nchini humo na katika Umoja wa Afrika.
Aidha Mheshimiwa Waziri amemsihi Balozi Shio kuhakikisha anasimamia misingi bora ya uhusiano mzuri uliyojengwa na waasisi wa mataifa haya mawili kwa manufaa mapana ya wananchi wa pande mbili ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
Kwa upande wake Mheshimiwa Balozi Shio amemshukuru Mheshimiwa Waziri kwa ziara hiyo fupi ya kujenga na kuimarisha ushirikiano na kuahidi kuyafanyia kazi kikamilifu maelekezo ya Mheshimiwa Waziri.




0 Comments