Na Omary Mbaraka
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Judith Kapinga (Mb) amesema Serikali chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan inaendelea kulinda ajira zilizopo na kuzalisha ajira mpya kupitia Viwanda na Biashara kwa manufaa ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Mhe Kapinga ameyasema hayo Leo mei 08,2026 Jijini Dar es Salaam alipotembelea Kiwanda cha Nguo cha Tooku Garments kilichopo Ubungo External na kubainisha kuwa ziara hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali kujiridhisha na Utendaji wa Viwanda nchini na kupanua wigo wa biashara.
Amesema Kiwanda hicho kimeajiri takribani Vijana 7,000,ambapo asilimia 75 ni Wanawake huku asilimia 60 ikiwa ni Vijana walio chini ya umri wa miaka 30.
Aidha waziri Kapinga amesisitiza kuwa Serikali inachukua hatua muhimu kutatua Changamoto zinazokikabili Kiwanda hicho na Viwanda vingine nchini ili kuboresha mazingira ya biashara.




0 Comments