Blog Post

WABUNGE WAUNGA MKONO KUJENGWA MUHIMBILI MPYA

 Na Mwandishi wetu 


Wakati Bunge likiendelea kujadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, baadhi ya wabunge wamejitokeza kuunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga Hospitali mpya ya Muhimbili, wakisema hatua hiyo ni muhimu katika kupunguza msongamano wa wagonjwa na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini.


Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalum (CCM),Mhe Asha Baraka, amesema ujenzi wa hospitali hiyo utakuwa suluhisho muhimu kwa changamoto ya msongamano mkubwa katika hospitali za rufaa, na utawezesha wananchi kupata huduma kwa ustarehe na ufanisi zaidi.


Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Mtwara, Mhe Asha Motto, amesema mpango huo ni chachu ya kukuza uchumi kwani utavutia wageni kutoka mataifa mbalimbali kuja kupatiwa huduma za kibingwa nchini.


Aidha, amesema mradi huo utaongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchochea ukuaji wa sekta ya afya na uchumi kwa ujumla.

Wakati huo huo utalii tiba pia itakuwa na kuliingizia pato serikali.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu