Blog Post

 Na Mwandishi wetu 


Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa mgombea mwenza wa urais mwaka 2025 kupitia Chama cha NCCR–Mageuzi, Dkt. Eveline Munisi, kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano.


Dkt. Eveline, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Mbunge, anachukua nafasi ya Rahma Kisuo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


Rais Samia pia amemhamisha Eliakim Chacha Maswi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum; huku Dkt. John Antony Jingu akihamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria.


Uteuzi na uhamisho huo umefanyika leo Jumamosi, Mei 2, 2026, na umetangazwa kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka


Post a Comment

0 Comments

Close Menu