Mfanyakazi aliyeungua moto wa kampuni ya Ravji Construction limited Bw Ramadhan Athumani Mdoe, amelalamikia Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) haikumtendea haki baada ya kupata ajali akiwa kazini.
Bw Mdoe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na blog hii kwa masikitiko makubwa.
Safari ya maisha ya maumivu, mashaka na ulemavu wa kudumu wa Bw Mdoe ambae alikuwa dereva wa mtambo wa kumwaga lami katika kampuni ya Ravji alianza kama ifuatavyo:r
Tarehe 5 Machi mwaka 2020 akiwa na bosi wake walikwenda katika eneo la kazi maeneo ya KIA mkoani moshi ambapo bosi wake alipanda katika mtambo wa kumwaga lami ujulikanao Asfat na yeye akiwa chini, bosi alibonyeza batani ambayo ilisababisha kupasuka kwa mpira uliokuwa na uji wa moto na kumuunguza vibaya bw Mdoe maeneo ya tumboni,mkononi na shingoni
Hivyo basi uongozi ulimkimbiza bw Mdoe katika kituo kidogo cha afya kilichopo maeneo ya Boma kijulikanacho Moshi specialist health centre, hata hivyo baada ya daktari kuona Mdoe kajeruhiwa vibaya alimuandikia rufaa kwenda KCMC moshi (tunayo kopi yake), hata hivyo uongozi wa Ravji Construction uliamua kumpeleka katika kituo kingine kidogo cha afya kilichopo moshi mjini kijulikanacho Siima healthy centre ambapo alitibiwa hapo kwa siku ishirini na nne.
Baada ya hapo uongozi wa Ravji Construction limited uliamua kumrudisha bw Mdoe nyumbani kwake Chanika Dar es salaam bila kumpa msaada wo wote wala mafao yake
Kwa vile alikosa matibabu ya kibingwa tumboni liliota gamba kubwa huku likiwa na matone mengi ya damu kama inavyoonekana katika picha juu.
Bw Mdoe alikuja katika chombo hiki cha habari wakati huo Tafakari Newspaper ambapo tulimsaidia kuyafikisha malalamiko yake kwa Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania ambae alitoa maelekezo katika ofisi ya waziri mkuu ambapo chombo hiki kinayo nakala ya barua hio
Kwa maelekezo hayo ndio WCF ilianza kumshughulikia na kumpeleka Muhimbili. Baada ya uchunguzi mkubwa madaktari wa muhimbili walitoa taarifa yao kuwa bw Mdoe ameumia sana ( severed injured) tunayo nakala
Pia madaktari wa WCF walimtazama na kutoa maoni yao ambayo bw Mdoe analalamika inawezekana hawakutoa taarifa sahihi kwani baada ya hapo ametelekezwa bila matibabu huku akiwa amepata ulemavu wa kudumu na bado gamba linazidi kukuwa huku likitoa damu
Hata hivyo baadae bw Mdoe alipata barua kutoka WCF kuwa atakuwa akipata t shs laki moja na sitini kila mwezi
Bw Mdoe anasema kwa hali alinayo sasa kawa na ulemavu wa kudumu hawezi kufanya kazi tena lakini inasemekana kama angepelekwa india kwa matibabu zaidi hasa plastic surgery ulemavu ungeondoka ama hata kama WCF ingenilipa kwa ajari kubwa niliopata na kwa ulemavu niliopata ningekwenda india kufanya plastic surgery alisema
Bw mdoe anasema mshahara aliokuwa akipata kama mtaalamu wa kumwaga lami ulikuwa ni shs laki tano na sasa anapata toka WCF shs laki moja sitini huku yupo na ulemavu mkubwa na ana mke na watoto wawili. Pia amedai hawezi hata kufanya tendo la ndoa tokana na ulemavu alionao.Anaomba msaada wo wote kwani madaktari wamemueleza kwa hali aliyonayo yupo hatarini kupata kansa
0 Comments