Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni, amesema kuwa sekta ya mafuta na gesi asilia nchini Tanzania ina fursa kubwa na zenye mvuto kwa uwekezaji, hivyo kuwahimiza wadau mbalimbali wa sekta hiyo
Mhandisi Sangweni amesema hayo Mei 14, 2026 jijini London, Uingereza, wakati akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi asilia nchini kwenye Kongamano la Nishati Afrika.
Akiwasilisha mada hiyo, Sangweni alibainisha kuwa miongoni mwa fursa zilizopo ni uwekezaji katika vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asili
Kinachosubiriwa kwa sasa ni kuidhinishwa kwa Mkataba Kifani wa Uzalishaji na Ugawanaji Mapato wa Mafuta na Gesi Asilia (Model Production Sharing Agreement – MPSA). Mara baada ya kuidhinishwa kwa MPSA hiyo, mchakato wa mnada wa vitalu utaanza mara moja,” alisema Sangweni.
Aidha, alieleza kuwa data mbalimbali za vitalu vilivyowazi zinapatikana kwa ajili ya wawekezaji kuziona na kuzinunua kwa madhumuni ya tathmini na uwekezaji. Miongoni mwa data hizo ni pamoja na data za nguvu sumaku ya miamba (magnetic), uzito wa miamba (gravity), mitetemo ya 2D na 3D pamoja na taarifa za visima.
Aliongeza kuwa utekelezaji unaoendelea wa miradi mbalimbali katika mkondo wa juu wa petroli, ikiwemo mradi wa uchimbaji wa visima vya uzalishaji wa gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay mkoani Mtwara, umeendelea kuongeza imani kwa wawekezaji na wadau wa sekta hiyo kuwekeza nchini Tanzania.





0 Comments