Blog Post

DANGOTE AKUTANA NA RAIS DKT SAMIA



Na Mwandishi wetu 


 Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote pamoja na ujumbe wake ikulu Dar es salaam 

Alhaji Dangote ni mmoja wa wawekezaji wakubwa Tanzania ambapo kiwanda chake cha saruji (Dangote Cement) mkoani Mtwara kinakuza uchumi wetu kupitia biashara ya saruji, ajira kwa Watanzania na kukuza sekta fungamanishi.

Katika kipindi hiki ambacho mataifa mengi duniani yanapambana kujenga uchumi kupitia uwekezaji mkubwa, Tanzania imeendelea kujijengea nafasi ya kipekee chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan kwa kutumia diplomasia ya uchumi inayolenga ushirikiano, utulivu na kujenga mazingira bora ya biashara. 


Ndiyo maana katika siku za hivi karibuni, mjadala uliofanyika Nairobi kuhusu uwekezaji wa mradi mkubwa wa kusafisha mafuta ghafi (refinery) unaodaiwa kutaka kujengwa Tanga ulivuta hisia za Watanzania wengi. Katika jukwaa hilo walionekana Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya William Ruto pamoja na mfanyabiashara mkubwa wa Afrika Aliko Dangote wakijadili mustakabali wa mradi huo wa kimkakati kwa ukanda wa Afrika Mashariki. 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu