Na Mwandishi wetu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaapenda kuuarifu umma kuwa leo Alhamisi, Mei 28, 2026 kesi ya mgawanyo wa mali za Chama iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili itaendelea kwenye Mahakama Kuu masijala ya Dar es Salaam.
Kesi hiyo itakayokuwa kwenye mahakama ya wazi kwa kesho inatarajiwa kusomwa hukumu ya uhalali wa kesi hiyo kuwepo mahakamani baada ya Mawakili wa Chama kuitaka
mahakama kuifuta kesi hiyo wakidai imefunguliwa nje ya muda.
Chama kinawaalika Wanachama, Watanzania, Jumuiya ya Kimataifa na wapenda haki kufika mahakamani ama kufuatilia kwa karibu kesi hiyo.
Imetolewa leo Alhamisi, Mei 28, 2026 na;




0 Comments