Blog Post

BALOZI DKT NCHIMBI AMWAKILISHA RAIS MSIBANI CHATO KESHO

 Na Mwandishi wetu 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Chato Mkoani Geita, ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Marehemu Bi. Suzana Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, yatakayofanyika tarehe 29 Mei 2026 Wilayani Chato.

 

Makamu wa Rais amepokelewa katika Uwanja wa Ndege Geita, Wilayani Chato, Mapokezi yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela, Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na Viongozi mbalimbali Waandamizi.

 

Pia Makamu wa Rais, amefika nyumbani kwa marehemu,Bi Suzana Magufuli, Kilimani Chato, kwa lengo la kusaini kitabu cha maombolezo pamoja na kuwafariji wafiwa kufuatia msiba huo.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu