Blog Post

RAIS DKT SAMIA AKUTANA NA RAIS KAGAME NA KUONGEZA USHIRIKIANO ZAIDI



 Na Omary Mbaraka 

Leo hii Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais Paul Kagame wa Ruanda wamekutana na kukubaliana kuzidi kushirikiana na kukuza biashara na uwekezaji walipokutana ikulu jijini Dar es salaam 

Hivyo wamekubaliana Kuondoa Vikwazo mbali mbali ambavyo havihusiani na kodi. Pia wakati Marais hao wakizungumza na waandishi wa Habari pia wamekubaliana mashirika ya umeme ya Tanzania na Ruanda kuwa na ushirikiano na kuuziana umeme, ili kuchochea zaidi maendeleo ya kiuchumi.

Makubaliano hayo yamezidi kuongeza fursa kubwa kwa wananchi wa pande zote mbili kuwekeza na hapo hapo fursa nyingi za ajira kupatikana wakati huo huo kukuza uchumi wa nchi.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu