Blog Post

RAIS MSTAAFU MHE KIKWETE ATOA MAFUNZO CHUO CHA HAVARD MAREKANI


 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, yuko jijini Boston, Marekani, ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo maalum kwa viongozi wa ngazi za juu kutoka mataifa mbalimbali yanayoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard.

Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Chuo Kikuu cha Harvard, yanalenga kuimarisha uwezo wa viongozi katika kusimamia sera na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika mataifa yao.


Katika programu hiyo, Dkt. Kikwete anashiriki kama mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu wenye uzoefu wa kipekee, akiwa na sifa ya kipekee ya kuwa aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Fedha kati ya mwaka 1994 na 1995 kabla ya kushika madaraka ya juu ya nchi.

Mafunzo hayo pia yameshirikisha Taasisi. mbali mbali za kimataifa ulimwenguni na mashirika binafsi bobozi kiuchumi

Tanzania imewakilishwa vyema katika mafunzo hayo na viongozi watatu waandamizi ambao ni Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar, pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo. Aidha, upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umewakilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Juma Malik Akil, ambapo kwa pamoja wanatarajiwa kunufaika na mbinu mpya za usimamizi wa mipango ya kitaifa.

Hii inaonyesha wazi  Tanzania tuna hazina  kubwa ya uongozi kutoka kwa Rais mstaafu Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu