Blog Post

MELI YA KWANZA YA UVUVI YAZINDULIWA NA RAIS DKT SAMIA

 Na Omary Mbaraka 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Jana Jumamosi, Aprili 25, 2026 amezindua rasmi meli ya kwanza ya uvuvi kwenye bahari kuu inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania.


Uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wadau wa sekta ya uvuvi walihudhuria.


Meli hiyo ni ya kwanza kwa serikali kuanza rasmi shughuli za uvuvi wa bahari kuu, hatua inayotarajiwa kuongeza uzalishaji wa samaki, kukuza uchumi wa buluu na kuongeza ajira kwa wananchi.


Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya uvuvi na kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa taifa.


Bahari kuu huhitaji meli maalumu kwa sababu mazingira yake ni magumu na ya hatari zaidi kuliko maeneo ya karibu na pwani. Kuna mawimbi makubwa, kina kirefu sana, umbali mkubwa kutoka nchi kavu, na hali ya hewa inayobadilika haraka.


Pia shughuli za uvuvi wa bahari kuu zinahitaji kukaa muda mrefu baharini na kushughulikia samaki wengi zaidi. Meli hiyo ni kubwa na imara ili kustahimili mawimbi makubwa.


Rais Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa meli ya kwanza ya uvuvi wa bahari kuu ni hatua muhimu katika kuimarisha uchumi wa buluu na kuhakikisha Watanzania wananufaika moja kwa moja na rasilimali za bahari.


Akizungumza Jana Aprili 25, 2026 katika hafla iliyofanyika Kigamboni, Dar es Salaam, Rais Samia amesema  uwekezaji huo unalenga kupunguza utegemezi wa meli za kigeni katika uvuvi wa bahari kuu na kuongeza uwezo wa nchi kuvuna rasilimali zake kwa manufaa ya ndani.


Ameeleza kuwa Serikali imejipanga kuendelea kuimarisha sekta ya uvuvi kupitia uwekezaji wa miundombinu, ununuzi wa meli zaidi pamoja na ujenzi wa bandari na viwanda vya kuchakata samaki, hatua zitakazoongeza ajira na kipato kwa wananchi.


Aidha, amebainisha kuwa maendeleo hayo ni sehemu ya mkakati mpana wa kukuza uchumi wa buluu, akieleza kuwa sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wananchi, hususan wa maeneo ya mwambao.


Katika hotuba yake, Rais Samia ametoa wito kwa taasisi husika na wadau kushirikiana kikamilifu kuhakikisha uwekezaji huo unaleta tija iliyokusudiwa, sambamba na kulinda rasilimali za bahari kwa matumizi endelevu.


Uzinduzi wa meli hiyo unaashiria mwanzo wa mpango wa Serikali kuwa na meli kadhaa za uvuvi wa bahari kuu, hatua inayotarajiwa kuiwezesha Tanzania kutumia kikamilifu rasilimali za bahari kwa maendeleo ya uchumi wake.


Uvuvi wa bahari kuu huhitaji meli maalumu kwa sababu mazingira yake ni magumu na ya hatari zaidi kuliko maeneo ya karibu na pwani. Kuna mawimbi makubwa, kina kirefu, umbali mkubwa kutoka nchi kavu, na hali ya hewa inayobadilika hapa


Rais Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa meli ya kwanza ya uvuvi wa bahari kuu unalenga kurejesha udhibiti wa rasilimali za bahari mikononi mwa Watanzania na kukomesha upotevu wa mapato uliokuwa ukinufaisha zaidi wageni.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa meli hiyo Jana Aprili 25, 2026, Rais Samia amesema kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikipoteza fursa kubwa za kiuchumi kutokana na uvuvi wa kina kirefu kufanywa na meli za kigeni, hali iliyosababisha mapato mengi ya sekta hiyo kwenda nje ya nchi.


Ameeleza kuwa uzinduzi wa meli hiyo mpya na ya kisasa ni ishara ya uthubutu na udhibiti wa uvuvi wa bahari kuu, huku akiwataka watendaji na wahusika kuhakikisha meli hiyo inalindwa na kutunzwa kwa maslahi mapana ya taifa.


Rais Samia amesisitiza kuwa uwekezaji wa meli hiyo pamoja na nyingine nne zitakazofuata ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kujenga uwezo wa ndani, kuongeza mapato ya taifa, kukuza ajira kwa vijana na kuwajengea wavuvi wa Tanzania uzoefu pamoja na ujuzi wa uvuvi wa kisasa.


Uzinduzi huo umefungua ukurasa mpya katika juhudi za Tanzania kujitegemea kwenye sekta ya uvuvi wa bahari kuu, huku Serikali ikiweka mkazo katika kulinda rasilimali, kuongeza mapato na kuhakikisha uchumi wa buluu unachangia zaidi maendeleo ya taifa.


Uvuvi wa bahari kuu huhitaji meli maalumu kutokana na mawimbi makubwa, kina kirefu, umbali mrefu na hali mbaya ya hewa. Meli iliyozunduliwa ni kubwa na imara, ikiwa na vifaa vya kisasa vya uvuvi kama sonar na radar, friza za kuhifadhi samaki, uwezo mkubwa wa mafuta na chakula, makazi ya wafanyakazi na mawasiliano ya uhakika.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu