Blog Post

MJUE BABA YAKE OBAMA

 Na Omary Mbaraka 

Baba yake na Obama aliekuwa RAIS wa Marekani bw.Barack Hussein Obama  Mwenye asili ya wa luo mzaliwa wa Kisumu Kenya


Mzee huyu Barack Hussein alikuwa ni mtu mwenye akili sanai toka utotoni hivyo ilipofika mwaka 1960 akitokea Chuo kikuu cha Nairobi Kenya alikwenda kusoma marekani Katika Chuo cha Hawaii na baadae Chuo kikubwa na maarufu nchini marekani cha Havard 

Mwaka 1961 alikutana na mwanamke  wa kimarekani na kumuoa Bi Ann Dunham na mwaka huo huo kumzaa aliekuwa Rais wa marekani Obama. Hata hivyo ndoa ya wazazi hao ilivunjika mwaka 1964

Muzee Barack Hussein aliwahi kukutana na mtoto wake  baada ya utotoni mara Moja alipofikisha miaka kumi

Baada ya kumaliza masomo yake bw Barrack Hussein na Kubobea na mambo ya uchumi alirudi Kenya na kufanya kazi serikalini na kuoa mke mwingine

 Hata hivyo Muzee huyu ambae alizaliwa mwaka 1936 alifariki mwaka 1982 kwa ajari ya gari pia kipindi hicho alikuwa na Hali ngumu ya kimaisha huku akinywa pombe nyingi

Post a Comment

0 Comments

Close Menu