Blog Post

MHE NCHIMBI AKEMEA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Na Omary Mbaraka 


ASISITIZA MALEZI BORA KWA WATOTO KWA MANUFAA YA TAIFA


APONGEZA JUKWAA LA TUZO ZA MALKIA WA NGUVU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameiasa jamii kukemea na kujiepusha na vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa kwa wanawake hususani katika mitandao ya kijamii.

 

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa kilele cha Tuzo kwa wanawake waliofanya vizuri katika sekta mbalimbali maarufu “Malkia wa Nguvu” kanda ya kati, zilizofanyika katika Ukumbi wa Mabele mkoani Dodoma. Amesema udhalilishaji huo unapaswa kukemewa na kila Mtanzania ili kusimamia heshima ya mwanamke katika jamii.

 

Makamu wa Rais amesema ni vema watanzania wote kuona wajibu wa kuilinda heshima ya mwanamke na kuwapima wanawake kwa majukumu yao yanayoleta maendeleo kwa Taifa. Amewasihi kipekee wanawake, kuacha tabia ya kushangilia katika mitandao ya kijamii hususani anapodhalilishwa mwanamke mwenzao.

 

Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wanawake nchini kwa kushirikiana na jamii kwa ujumla kuchukua hatua katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa watoto. Amesema imekuwepo tabia ya watoto kujiingiza katika matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiwekwa maudhui yasiyofaa hivyo kuharibu maadili na kuhatarisha kizazi cha sasa na kijacho.

 

Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kusimamia mambo yatakayoleta mabadiliko kwa wanawake ikiwemo kuendeleza majukwaa ya uwezeshaji ikiwemo mpango wa 2022-2032 na kusimamia mfuko wa maendeleo ya wanawake ambao unahusika na ukopeshaji.

 

Pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kujenga maendeleo ya nchi kuinua ajira na kutengeneza fursa pamoja na kuzingatia nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa Taifa. Ametoa wito kwa Jukwaa la Malkia wa Nguvu kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu na hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

 

Makamu wa Rais amewapongeza wanawake katika kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Taifa na shughuli za maendeleo kwa ujumla. Amesema nia ya Serikali kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni kujenga Taifa lenye nguvu kwa kujengea uwezo watu wake kwa kuz

               

Post a Comment

0 Comments

Close Menu