Blog Post

DKT MATARAGIO ASEMA MAFUTA YANATOSHA MPAKA JULAI 2026


 Na Omary Mbaraka 

Katibu mkuu wizara ya nishati Dkt James Mataragio na wawakilishi wakuu kutoka TRA na EWURA Jana walitembelea katika hifadhi (depot's) za Mafuta ya dizeli na petroli na kusema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha Mafuta hayo yatatosheleza  mpaka julai 2026 pia kuagizwa mengine kuanzia August 2026 na kuwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi watulie

Ambapo mwakilishi wa TRA alisema atahakikisha taratibu zote zitafanywa haraka ili Mafuta hayo yawafikie haraka walaji kutoka bandarini mpaka katika vituo vya mafuta

Nae meneja mkuu wa Camel oil bw Saleh Bajber  akiwakilisha sekta binafsi alisema wanayo hifadhi ya kutosha ya Mafuta na wanajiandaa vizuri kwa miezi 2 mpaka 3 kuhakikisha wanasambaza vizuri katika vituo vya mafuta ili walaji wapate huduma stahiki

Bw Bajber alisema kwa mwezi wa April 2026 watapata Lita milioni 70 kwa ajili ya vituo vyao vya mafuta na kwa mwezi may 2026 tayari wameagiza zaidi ya Lita milioni 84 wakati huo hio alisema mwezi machi 2025 tayari walipokea Lita milioni 44

Nae katibu mkuu wa chama Cha wamiliki wa vituo vya mafuta nchini TAPSOA  bw Tino Mmasy alisema wanachama wake wanafanya kazi kwa ushirikiano mazuri na Serikali hivyo wananchi wategemee huduma nzuri 

..,

Post a Comment

0 Comments

Close Menu