Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewatembelea na kuwajulia hali Mama Salma Omar Ali Juma, mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam na Mama Regina Lowassa, mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Masaki pia kwa mama Anna Mkapa Jijini Dar es Salaam janaJanuari 22, 2026.






0 Comments