Na Omary Mbaraka
Mbunge wa Jimbo la Makunduchi, Mhe. Wanu Hafidh Ameir katika ziara yake jimboni humo ya mnamo Desemba 28, 2025 amewakabidhi vifaa vya kilimo aina ya Nyuzi na Taitai kwa wakaazi wa Shehia ya Kajengwa kwaajili ya kuwasadia katika shughuli zao za Kilimo cha Mwani, ikiwa ni sehemu ya ahadi alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.
Mhe. Wanu amekabidhi mipira Nyuzi 450 na Taitai 900 na kuahidi kuongeza zaidi pale itakapohitajika, ambapo pia ameendeleza mfululizo wa mikutano kwaajili ya kutoa shukrani na kupokea maoni, ushauri, mapendelezo na kero kutoka kwa wakaazi wa Jimbo la Makunduchi, ambapo mpaka sasa amekwishatembelea Shehia za Mtende, Kajengwa na Muyuni A.



0 Comments