✍️🇹🇿🤝HAPPY BIRTH DAY 🎂 🎉 🎂 MHE RAIS SAMIA:WATANZANIA TUMUUNGE MKONO KWA KUPANDA MITI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan January 27,2026 ni siku yake ya kuzaliwa. Hongera Mhe Rais kwa kuongeza mwaka mwingine tena. Ni hakika Mungu ni Mwema hivi waliokuwa wanatabiri tunasema acheni uongo mmeamini Mungu sio Mwanadamu na mmetambua mnautumia Imani vibaya?? Maisha ni Mungu anajalia tena zaidi ya Mwanadamu na Mwanadamu akiwaza mabaya Mungu hujifunua kwa wema kwa unayemwazia mabaya ili ujue Mungu si Mwanadamu
Mhe Rais, Sisi Watanzania tunakutakia afya njema na uwe na maisha marefu pia ili uendelee kuitumikia Nchi yako Tanzania kwa moyo na khari kubwa ili tufikie malengo yetu tuliojiwekea ya Tanzania ya kazi na utu tukisonga mbele katika sekta zote ikiwemo Elimu na Afya Umejalia NCHI kuweka Historia kubwa ya Elimu kuwa jibu la tatizo la ajira baada ya mabadiliko na Maboresho ya Sera na mtaala na Bima ya Afya kwa wote haya ni sehemu ya amezaliwa mtu Bora kwa Jamii na Taifa la Tanzania.
Naamini tuendako bima ya Afya kwa wote itatozwa In direct watanzania waondokane na kutoa wao kama wao chanzo cha mapato kinachowagusa wote kutozwa Afya na Elimu hata 1% ili Elimu ya Amali na Matibabu iwe ni hakika watanzania wote wanaipata bila changamoto zao binafsi za kutomudu.
Katika siku yako ya kuzaliwa January 27,2026 ,Mhe Rais umeona vyema iweke historia kwa kupanda miti maeneo ya Kizimkazi na Bungi Kilimo, Zanzibar na Tanzania bara watanzania wote kupitia wito huu ikiwa ni sehemu ya ajenda yako muhimu ya kitaifa ya kulinda mazingira, kulinda vyanzo vya Maji na kukabiliana na matishio ya mabadiliko ya tabia Nchi.
Zoezi hili linaongozwa na kauli mbiu: Uzalendo ni Kutunza Mazingira,Shiriki Kupanda Miti.
Watanzania wote kwenye Mikoa na Wilaya zote Nchini hebu tumuunge mkono Mhe Rais Dkt Samia katika zoezi hili kwa kushiriki kupanda miti kwa ajili ya afya ya mazingira yetu tena katika nyakati za furaha ya kuzaliwa kwake.
HEBU TUJIFUNZE PIA KWA WENZETU WANACHOFANYA
👇🏾👇🏾👇👇👇
Mwaka 2020, Rais wa Marekani wakati huo Donald Trump alitangaza Marekani kujiunga na mpango wa dunia(World Economic Forum's One Trilion Trees Initiative) kwa kupanda miti trilioni moja duniani kufikia mwaka 2030.
Waziri Mkuu wa Ethiopia mwaka 2019 alitangaza kuanzisha kampeni ya kupanda miti bilioni 40 kufikia mwaka 2025 kupitia kampeni yake ya Ethiopia's Green Legacy Initiative.
Jirani Wiliam Ruto,Rais wa Kenya,pia alitangaza kampeni ya kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032 kupitia kampeni yake ya Kenya's 15 Billion Trees Campaign.
Huo ndio uelekeo wa dunia kwahiyo Watanzania tunaombwa kushiriki zoezi hili muhimu bila kukosa katika maeneo yetu Nchi nzima ifikapo January 27,2026.
Kwa mara nyingine tena ,Happy BirthDay Mh Rais Samia Suluhu Hassan.



0 Comments