Na Omary Mbaraka
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkono ujenzi wa stendi ya daladala ya Bunju B iliyopo Kata ya Mabwepande, ujenzi utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.3.
Akiongea wakati wa ziara aliyoifanya leo Disemba 29, 2025, wakati akitembelea Soko la Bunju B pamoja na kusikiliza kero za Wananchi, Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amesema kuwa amepokea wazo la uhitaji wa ujenzi wa stendi ya daladala na ameahidi kuwa hitaji la fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.3 ili kukamilisha Ujenzi wa Stendi hiyo kwa Haraka.
"Nakubaliana nanyi na nnaunga mkono ujenzi wa stendi hii kwani utakwenda kuongeza kasi na Mzunguko wa biashara katika eneo hili la Bunju” amesisitiza Dkt. Nchemba.
Aidha, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa stendi hiyo ya daladala itakayoenda sambamba na miundombinu ya barabara, soko na maduka iandaliwe kwa mazingira ya kusaidia na kuondoa kero za usafiri na biashara kwa Wananchi.



0 Comments