Blog Post

USHINDI CCM UTAANZA NA WAJUMBE MAKINI KUCHAGUA VIONGOZI BORA -RIDHWANI KIKWETE







 Na Omary Mbaraka 

Mgombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete, amewaasa wanachama viongozi ambao ni wajumbe wa mkutano Mkuu wa Jimbo kuwa makini katika kuchagua na haswa wakijua kuwa ushindi wa Chama Cha Mapinduzi unawategemea na kuwa wachague viongozi bora

Maneno hayo ameyasema wakati akizungumza na wajumbe hao katika kata za Ubena, Msoga, lugoba na Msata. Katika mikutano hiyo ambayo pia inalenga kuwatambulisha wagombea nafasi za udiwani na imetumika pia kuwakumbusha viongozi hao juu ya majukumu makubwa waliyonayo ya kutangaza mazuri yaliyokwishafanywa katika miaka mitano ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Mgombea kikwete alitumia hadhira hiyo kuwakumbusha mafanikio waliyokwisha yapata katika Sekta mbalimbali ikiwemo miundoMbinu ya Barabara, Afya, Elimu , Maji, uwezeshaji wananchi, maendeleo ya Jamii na kadhalika. 

Vikao hivi vinahitimishwa kwa kufanyika kwa zoezi la kupiga kura kuchagua Madiwani na kumthibitisha Mgombea Ubunge wa jimbo hilo ambaye amepita bila kupingwa tarehe 14 Agosti 2025.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu