Na Omary Mbaraka
Kumuombea dua kiongozi wa nchi yetu Dkt, Samia Suluhu Hassan, ni kitendo cha kiungwana na uzalendo kwa nchi, ambacho kimekuwa kikifanywa kwa miaka mingi hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mh. Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Mhe Ridhiwani ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia Wananchi waliojitokeza kuomba dua kuiombea nchi na kiongzi wa ncini Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoa wa Pwani.
Akizungumza na umma wa Watanzania waliojitokeza kwenye dua hiyo, Mh. Kikwete amewashukuru kwa kujitokeza na kumuombea dua Mh. Rais. “ ukimuombea Rais Samia, umeiombea Tanzania, kutokana na umuhimu wa nafasi yake na yeye akiwa ndiyo mshika maono ya Nchi”. Mh. Kikwete alisema na alitumia nafasi hiyo pia kuishukuru serikali ya awamu ya 6 kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hii ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Elimu,Afya, Miundombinu n.k na kutumia nafasi hiyo pia kuwaomba wanachalinze waendelee kumuamini na kumchagua tena kwa kura nyingi.
Tukizungumza na baadhi ya masheikh waliohudhuria shughuli hii, wamepokea maombi ya Mbunge wao kwa furaha na hivyo watatekeleza kwa ari kubwa.
Dua na Futari ni utaratibu ambao Mbunge wa jimbo la Chalinze amekuwa anafanya kila mwaka kipindi hiki cha Mfungo wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
0 Comments