Blog Post

MFANYABIASHARA MANZESE ANAINGIZA NCHINI MAFUTA KWA MAGENDO


Na Mwandishi Wetu 

Mfanyabiashara mmoja Manzese jijini Dar es Salaam, (jina tunalihifadhi kwa sasa), anajihusisha na kuingiza bidhaa za mafuta ya kula kwa njia za magendo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, mfanyabiashara huyo anamiliki duka kubwa la jumla na rejareja la bidhaa za vyakula maeneo ya Manzese. 

Mfanyabiashara huyo ambaye anajificha sana akimtumia mpambe wake katika shughuli zake, anaingiza mafuta ya kula kwa njia za panya kupitia bandari ya Bagamoyo bila kulipa ushuru.

Hivi karibu alikamatwa na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Nchini TRA, na gari aina ya canter ikiwa na madumu zaidi ya 600, yakiwa yameingizwa kwa magendo bila kulipiwa ushuru.

Baada ya maafisa hao kukamata mzigo huo ulipelekwa yadi ya TRA Ubungo kwa uchunguzi zaidi.

Juhudi za kumtafuta mfanyabiashara huyo na taarifa kamili kutoka TRA zinaendelea, watakapopatikana tutaweka wazi taarifa kamili.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu