Blog Post

WALIOOMBA AJIRA TRA WAITWA KWENYE USAILI MACHI 29 NA 30 2025



 Na James Nyanda Malwilo 

Mamlaka ya mapsto Tanzania (TRA) tarehe 6 February 2025 ilitangaza nafasi 1596 za kazi katika fani mbali mbali na kutoa muda wa siku 14 za


kupokea maombi ya kazi. Hata hivyo kufikia saa sita usiku tarehe 19 February Mamlaka hio ilipokea maombi 135027 alisema mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya mapsto Tanzania (TRA).Bw Moshi Jonathan Kabengwe

Baada ya hapo TRA ilipitia maombi hayo na kupata maombi 112952 yaliyokidhi vigezo ambao watahudhuria katika USAILI wa maandishi( Written interview) utakaofanyika tarehe 29 na 30 March 2025, majina ya hao watahiniwa yametangazwa tarehe 22 March 2025 ama yanapatikana katika mtandao wa TRA wa www.tra.go.tz alisema bw Kabengwe

Bw Kabengwe alisema pia usaili huo wa mchujo utafafanyika katika vituo tisa hapa nchini ambalo maelekezo tayari yametolewa kwa watahiniwa ikiwa kituo alichopangwa,muda nk.Vituo hivyo ni kama ifuatavyo;

1 Dar es salaam kwa mikoa ya Pwani na Dares salaam 

2 Zanzibar kwa Unguja na Pemba

3 Arusha kwa Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Arusha

4 Dodoma kwa Morogoro,Singida, Iringa, Tabora na Dodoma

5 Mtwara kwa Lindi, Ruvuma na Mtwara 

6 Mbeya kwa Songwe,Rukwa na Mbeya

7 Mwanza kwa Shinyanga, Simiyu na Mwanza

8 Kagera kwa Geita na Kagera

9 Kigoma kwa Katavi na Kigoma

Bw Kabengwe amesema pia kwa waombaji wenye mahitaji maalum watawekewa mazingira maalumu ambayo yatawasaidia kufanya usaili bila usumbufu

Post a Comment

0 Comments

Close Menu