Vijana wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uhakiki wa Rasimu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kutoa maoni yanayowagusa ikiwemo kubainisha mambo ambayo Dira hiyo haijayazungumzia pamoja na kushauri maboresho yanayopaswa kufanyika ili kuhakikisha kuwa masuala yao yanawasilishwa ipasavyo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mgeni rasmi, katika Mkutano na Mtandao wa Vijana Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaofanyika jana Jumatano Desemba 18, 2024 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam.
“Lazima wajue (vijana) kama kuna maeneo ambayo hayakusemwa vizuri, ni nafasi yenu vijana kueleza kwa uwazi zaidi na hili muwe wakweli zaidi hilo ni la kwanza. La pili, kwenye uhakiki yako maeneo ambayo tunadhani hayakuelezwa vizuri, ni nafasi yetu pia kueleza vizuri,” amesisitiza Ridhiwani.
0 Comments