Blog Post

MAMLAKA ZA UJENZI ZAENDELEA KUPUUZWA







Na Ismail Mang'ola, Dar

UJENZI wa majengo ya ghorofa moja na kuendelea ambayo pia hudhaniwa kuwa hayana ubora kwa kukosa vigezo mbalimbali Kama vile, Usajili wa mradi, Wakandarasi pamoja na wahandisi waliosajiliwa na Bodi husika yameendelea kujengwa na kuzagaa jijini Dar es Salaam.

Chombo hiki cha habari kilipata taarifa hizo na kutembelea maeneo mbalimbali katika Jiji Hilo na hasa baada ya tukio lie la  kuporomoka kwa moja ya maghorofa eneo la Kariakoo na kuua pamoja na kujeruhi watu zaidi ya 80.

Hii imethibitika kwa waandishi hao waliojikita hasa kuandika habari za makazi na mazingira na kujionea wenyewe maeneo ya KIMARA Stop Over, Kigogo na hata eneo la Kata ya Mabibo mtaa wa Shoka kuliona jengo linaloendelea kujengwa kwa sasa likiwa ni la ghorofa mbili ambalo linaenda hadi ghorofa tatu.

 Alipoulizwa fundi Mkuu ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake lichapishwe na chombo hiki wala Mhandisi alisema, " ni kweli tunajenga jengo na ni la ghorofa tatu lakini mimi sio msemaji labda niwapatie namba ya mmiliki huyo ndiye mnaweza kumuuliza maswali yenu na atawajibu ambaye ni bw. Munisi", alisema fundi huyo na kutoa namba zake za simu. 

Bw. Munisi alipopigiwa alisema hajui lolote nje ya kuambiwa ajenge au asimamie labda nendeni Ukonga Gerezani kuna Bosi mmoja ndiye mmiliki wa jengo hilo lakini hata hivyo hakutuma namba hizo mazingira ambayo  yanayoonesha kutia Shaka kuwa ana lengo la kuwatisha Waandishi wa habari hizi.

Toleo lijalo tutawaletea ukweli wa mmiliki halisi, Mkandarasi (Contractor) na Mhandisi (Engineer) kwani ni jengo lisilokuwa na Bango ( Signboard) na hata vitendea kazi (PPE).mpaka hivi Leo tulipolitembelea

Post a Comment

0 Comments

Close Menu