Na Omary Mbaraka
Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira, na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunga mwaka na Bonanza kubwa la Chalinze Festival Leo Jumanne Disemba 31, 2024 kwenye Uwanja wa Polisi Chalinze lililofanyika kuanzia majira ya saa 9 alasiri. kabla ya bonanza hilo kuanza Waziri Kikwete aligawa vifaa kwa ajili ya Bonanza hilo
Ilifanyika michezo miwili mikali kati ya Chalinze United Vs Mdaula United na ule wa Watumishi CDC HQ Vs Wasanii Bongo Movie. Mgeni rasmi kwenye Bonanza hili la aina yake alikuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Zifuatazo ni picha za waziri Kikwete alipokuwa aligawa vifaa mbali mbali
0 Comments