Blog Post

MBUNGE CHALINZE AANZA MWAKA KWA DUA




Na Ismail Mang'ola

WAZIRI wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Ajira kazi na watu wenye ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhwani Kikwete, ameuanza mwaka 2015 kwa kuomba dua.

Mhe. Kikwete ameuanza mwaka huu kwa kumombea Dua RAIS WA Jamhuri ya Muungano WA TANZANIA Dkt. Samia Suluhu Hassani pamoja na TAIFA kwa ujumla.

"Tumepata nafasi ya kuomba Dua ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi nyingi alizotujaalia katika maisha yetu. Tumemshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uhai , Afya na Neema alizotujaalia. Haya sio kwa Ujanja wetu ni kudra yake". Amesema Mhe. Kikwete.

Aidha Mhe. Kikwete, ameendelea kusema kuwa, kufanya hivyo ni kwa ajili ya Mhe. Rais ambaye ameonyesha umahiri mkubwa katika uongozi wake wenye mashiko na wenye kujali maslahi ya wananchi wake.

"Tumemshukuru Mwenyezi Mungu  kwa ajili ya Rais wetu, Dr. Samia Suluhu Hassan. Tumemshukuru na kumuombea Mh. Rais kwa Uongozi wake wenye mashiko na unaojali wananchi wake. Maendeleo tuliyoyapata, mafanikio yetu kama 

Nchi, Utulivu, Amani , na Mshikamano uliopo yote ni kazi yake Mh. Rais kwa Neema na Vipawa alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu. Tunakushukuru Sana Mh. Rais tunapoukaribisha Mwaka mpya na kuendelea kukuombea Mungu". Alisema Mhe Kikwete 

"Pia tunawaombea kheri wazee wetu, wazazi wetu, watoto na wake zetu . Allah awape huruma, mapenzi , na Malezi mema ili tuendelee kukua na kuleana pamoja". alisema Mhe Kikwete 

"Tumeiombea Nchi, kupatikane utulivu, Idumu amani na Upendo baina yetu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jema analotujalia. " Alisema Mhe Kikwete 

Mwenyezi Mungu atulinde sote na kutujalia amani na utulivu ,Mwenyezi Mungu ilinde Tanzania, Mwenyezi Mungu mlinde Rais Wetu.aliongeza Mh Kikwete.Pia katika hafla hio nzito ilihudhuriwa na Rais mstaafu Mhe dkt Jakaya Mrisho Kikwete 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu