Blog Post

RIDHIWANI ATOA RAI LESCO KUENDELEA KUZINGATIA MISINGI KAZI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameitaka bodi ya Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO), kuhakikisha sekta ya ajira inazingatia misingi ya kazi.

Mhe. Ridhwan ametoa raid hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na kuwapongeza  bodi ya Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO) kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yao wanapoelekea kumaliza muda wao wa Miaka Mitatu ya Kazi, leo Septemba 5, 2024 jijini Dodoma.

Pamoja na kuwapongeza alitoa rai kwa wajumbe wa baraza hilo kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuhakikisha sekta ya kazi na ajira inazingatia misingi ya kazi zenye staha kwa maslahi ya wafanyakazi na waajiri.

Awali, Mwenyekiti wa LESCO Dkt. Samwel Nyantahe ameishukuru serikali kwa kutoa ushirikiano katikia kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao.

Uongozi wa Baraza hilo unamaliza muda wake Septemba 12, 2024 na kwasasa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza mchakato wa kuwapata wajumbe wengine.



Post a Comment

0 Comments

Close Menu