![]() |
Na Ibrhim Kadilo Mradi mkubwa wa ujenzi unatarajiwa kujengwa maghala makubwa ya kisasa maeneo ya Yombo Buza unajengwa bila kusajiliwa kwenye bodi zinazosimamia ujenzi hapa nchini |
![]() |
Mradi huu wa ujenzi unakadiriwa kugharimu mabilioni ya shilingi unajengwa wakati eneo la mradi hakuna bango linaloonesha ni kampuni gani inajenga mradi huo |
Na Waandishi Wetu
Mradi mkubwa wa ujenzi unajengwa na mafundi wa mtaani ambao hawana vitendea kazi na haujasajili kwenye bodi husika za ujenzi.
Mradi huo unajengwa na Injinia aliyefahamika kwa jina la Abdulazak kutoka kampuni ya Multi Cable Tanzania ambaye alipoulizwa alisema yeye hawezi kuzungumzia suala hilo.
Mwanasheria wa kampuni hiyo alipoulizwa ofisini kwake alisema kuwa ni kweli hawajasajili mradi huo kwenye bodi husika kwa sababu huo ni ujenzi wa uzio tu hahuitaji usimamizi wa bodi za ujenzi hapa nchini wala kulipia usajili wa mradi kwenye bodi hizo.
Alisema wamefanikiwa kupata kibali cha ujenzi mdogo kwenye manispaa na hawalazimiki kusajili mradi huo kwenye bodi husika.
Kuhusu suala la wafanyakazi kufanya kazi bila kuwa na vitendea kazi alisema kuwa hilo ni suala linamuhusi injinia anyesimamia mradi na sio kampuni yako.
Blogo hii inaendelea kumtafuta msajili wa bodi ya CRB kuzungumzia ujenzi huo unaofanya kwenye eneo la Chama ch Mapinduzi CCM kuwa hahutaji kusajiliwa kwenye bodi za ujenzi na serikali kupata mapato.
0 Comments