Blog Post

KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI GAZETI LA ZAMANI LA MFANYAKAZI LAZINDULIWA

Na Omar Mbaraka Katika sherehe za kuadhimisha siku ya wafanyakazi mei mosi zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa sheikh Amri Abeid leo jijini Arusha, mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe dk Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe Dk Philip Ididori Mpango amelizindua rasmi gazeti la zamani la Mfanyakaxi Gazeti la zamani la mfanyakaxi lilikuwa likichapishwa na chama cha wafanyakazi OTTU wakati huo likiwa na waandishi mahili na nguli akiwemo mhariri mkuu Hemed Kimwanga na mwandishi Charles Charles ambao wote baadae walihamia gazeti la Tafakari baadae Charles Charles aliwahi kuwa katibu wa CCM wilaya ya Pangani Gazeti hilo lilivuma sana na kupendwa sana kwa kipindi hicho ambalo lilikuwa likitoka kila jumamosi

Post a Comment

0 Comments

Close Menu