Blog Post

Wakandarasi wa umeme wanaosuasua kukiona

 




Na Mwandishi Wetu

Mkandarasi wanasuasua kutekeleza miradi ya umeme kuchukuliwawa hatua kali, na kutakiwa kutokufumbiwa macho, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga awajia juu.

Mhe.  Judith Kapinga  amewataka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kutobeba changamoto za wakandarasi wabovu na wanaolegalega katika kutekeleza Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini  badala yake wawachukulie hatua kwa mujibu wa mikataba uliowekwa

Mhe. Kapinga amesema hayo tarehe 6 Desemba, 2023 wakati wa ziara yake mkoani Tanga ya kukagua Maendeleo ya Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini katika Wilaya ya Korogwe, ambapo pamoja na mambo  mengine ameeleza kuwa REA na TANESCO wakibeba changamoto hizo, inasababisha wananchi kufahamu kuwa wao ndiyo wenye matatizo.

Mhe. Kapinga amelazimika kusema hayo kufuatia kuwepo kwa mkandarasi wa Kampuni ya TONTAN kutounganisha umeme katika baadhi ya vijiji na vitongoji vya  Wilaya ya Korogwe Vijijini kwa sababu mbalimbali.

Amesema Serikali imejitahidi sana kumsimamia huyo mkandarasi, imekaa naye mara nyingi ili kuona atamaliza lini kazi, lakini mkandarasi analegalega na siyo muungwana kwa sababu amepewa kazi ya kuunganisha watanzania ambao wanamahitaji ya umeme ili kuboresha hali zao za kiuchumi na bado ameendelea kulegalega  hivyo hawatendei haki watu hao kwa sababu wanataka umeme ili waboreshe maisha yao. 

"REA na  TANESCO acheni kubeba changamoto za wa kandarasi wabovu na wanaolegalega kwa kuwa wananchi wanaona kuwa ninyi ndiyo wenye shida, msiwakingie vifua wala kuwatatulia changamoto zao hayo siyo matatizo yenu ni matatizo ya mkandarasi asiye muaminifu na hatutakubali  mkandarasi mbovu aturudishe nyuma" Amesema Mhe Kapinga 

Mkandarasi huyo alitakiwa kumaliza kazi desemba  30 mwaka huu, lakini mpaka sasa takribani siku 24 zimesalia mkandarasi huyo bado hajamaliza kazi, hivyo amewataka REA kutompa kazi tena Mkandarasi huyo hata kama atamaliza kazi hiyo kwa muda uliosalia na Serikali iko kazini kuhakikisha mkandarasi huyo anatekeleza kazi yake kwa mujibu wa mkataba. 

Amewataka Wakandrasi kuacha tabia ya kusingizia mvua, barabara mbovu ama eneo la milimani kwakuwa wakati wakipewa mkataba wa kazi hayo yote yalifahamika.

 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu