Blog Post

SERIKALI IMESEMA ITAZINGATIA HALI YA HEWA NA KILIMO KUKUZA UCHUMI

 


Na Mwandishi Wetu

Serikali imesema kuwa inaweka kipaumbele cha kwanza kwenye kilimo kinachozingatia hali ya hewa na mazingira kukuza uchumi wa taifa na kipato cha wananchi wake.

Hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibra, Dkt. Husein Mwinyi alipokuwa kwenye mkutano akimwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kimataifa wa tathimini ya muda wa kati wa mzunguko wa 20 Benki ya Dunia.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi , amesema Tanzania imeweka kipaumbele kwa kuongeza  uwekezaji katika elimu, afya, na huduma nyingine za kijamii pamoja na kilimo kinachozingatia hali ya hewa na mazingira.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo  akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt Samia Suluhu Hassan, alipofungua Mkutano wa Kimataifa wa Tathmini ya muda wa kati wa mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia(IDA20 Mid Term Review) unaofanyika hoteli ya Golden Tulip uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 06 Desemba 2023.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa kuongozwa na falsafa ya 4R ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayohusu mambo manne ya msingi ya kuzingatiwa ambayo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na ujenzi mpya.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu