Baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuagiza wizara ya ujenzi kuhakikisha mji wa Katesh inarejea katika hali yake ya kawaida.
Waziri wa
Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope inaendelea na shughuli
kubwa inayofanyika kwa sasa ni kufungua mitaa yote ya mji wa Katesh na
kurejesha mji katika hali yake ya awali kwa kuwezesha shughuli za uzalishaji
kuendelea.
Ameyasema hayo mapema asubuhi hii wakati wakikagua kazi zilizofanyika ambapo aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama, Waziri wa Madini, Antony Mavunde na Viongozi wengine , leo tarehe 6 Disemba 2023.
“ *Maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha leo kufikia usiku, mji wa Katesh na mitaa yake iwe imesafishwa ili kushughuli za uzalishaji ziendelee kama mnavyoona Wafanyabiasha wameanza kufungua Maduka* ” amesema Bashungwa
Bashungwa
amesema TANROADS kwa kushirikiana na TARURA tayari ameweka mpango kazi wa
pamoja ambao utahakikisha kazi hiyo
inaendelea kufanyika usiku na mchana mpaka shughuli hiyo itakapokamilika.
0 Comments