Blog Post

DKT MWINYI AFUNGUA KIKAO CHA 77 CHA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA ARUSHA





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi aliondoka jana  Zanzibar na kuwasili Jijini Arusha ambapo leo tarehe 20 Oktoba 2023 amefungua kikao cha 77 cha Kamisheni ya Umoja wa Afrika kinachohusu haki za binadamu na watu atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC.

Katika uwanja wa ndege wa Arusha alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella , Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Pindi Chana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba , Sheria , Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman pamoja na viongozi mbalimbali wengine wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha na vyombo vya ulinzi na usalama.



📍Arusha.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu