Blog Post

Rais Samia azindua Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini



Na Mwandishi Wetu, MTWARA

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan mapema amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara leo Septemba 15, 2023.

Rais Samia amesema kuwa kukamilika kwa Hospitali hiyo ambayo ina watalaam, vifaa na vifaatiba vya kisasa itasaidia watu wa Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kupata uhakika wa huduma za matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.

“Wagonjwa wote wenye matatizo makubwa watakuja hapa, jengo hili litumike kutoa huduma za afya” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa kazi ya watumishi wa afya ni kuokoa maisha ya watu hivyo watumishi hao wajitume kufanya kazi kwa kuwa Serikali imewekeza kwenye miundombinu, vifaa na dawa na wao watimize wajibu wao. 

"Tunahitaji matunzo ya jengo hili, vifaa na huduma kwa wananchi kwa lugha nzuri, kila mtu amepangiwa jukumu lake na Mwenyezi Mungu, tumridhishe Mungu kwa huduma tunazozitoa, nawatakia kila la kheri” amesema Rais Samia huku akiongezea kuwa changamoto zilizopo za watumishi zitaendelea kufanyiwa kazi kwa haraka.

Katika hatua nyingine Dkt. Samia amefanya kazi ya maboresho yanayofanyika uwanja wa ndege wa Mtwara. 

Rais Samia alipata maelekezo ya ukaguzi huo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari wakati alipowasili uwanja wa ndege wa Mtwara na kufanya ukaguzi wa maboresho yanayofanyika uwanjani hapo.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu