Blog Post

KITUO CHA AFYA MSATA CHAANZA UPASUAJI


Na Omar Mbaraka

KITUO cha Afya cha Msata katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani kimeanza kutoa huduma ya Upasuaji.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze. ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema hizo ni taarifa njema. 

"Nimepokea habari njema toka Halmashauri yetu ya Chalinze kwenda kwetu Wananchi, kwamba kituo chetu cha Afya Msata kimeanza upasuaji tarehe 14/09/2023", ameandika Mheshimiwa Ridhiwani katika andiko lake kwenye Ukurasa wake wa Instagram jana.

Hayo ni Mapinduzi mengine makubwa kwa Wananchi wa eneo hilo kwani mwaka 2018, wakati huo ikiwa Zahanati, ilipata na ushindi wa kimkoa   baada ya kufanya vizuri katika utoaji huduma za afya kwa wananchi kwa kuzingatia matokeo makubwa sasa (BRN) na kufanikiwa kupata nyota nne kati ya vituo vyote vya afya katika mkoa wa Pwani.

Ushindi huo ulipatikana  kutokana na ukaguzi uliofanywa na wizara ya Afya kwa ajili ya malipo kutokana na matokeo ya huduma kwa matokeo makubwa sasa na Zahanati ya Msata ilionekana kukidhi vigezo vilivyowekwa na wizara ya Afya kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia matokeo makubwa sasa.




Post a Comment

0 Comments

Close Menu