Blog Post

TUTAENDELEA KUYAPA KIPAUMBELE MASLAHI YA WATUMISHI-KIKWETE



Na Omar Mbaraka


SERIKALI imesema itaendelea kuyapa kipaumbele maslahi ya watumishi wake ili kuimarisha utendaji wao kazini sambamba na kuboresha maisha yao.

Hayo yamesemwa katika mkutano na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi -Manyoni, Singida na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Jakaya Kikwete  kwenye ziara ya kikazi mkoani hapo. 

Akizungumza na Watumishi waliojaa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, Naibu Waziri wa Utumishi aliwakumbusha hatua mbalimbali zilizofanywa na serikali kutatua kero mbalimbali za watumishi ikiwemo kero ya kutopanda madaraja kwa muda mrefu, madai ya malimbikizo ya madeni na mishahara na kupanda vyeo na maskahi mengineyo. 

Akizungumzia mbele ya Watumishi hao amewaambia kuwa katika mwaka uliokwisha wafanyakazi zaidi ya 454,508  wamepandishwa madaraja, watumishi 101,651 wamebadilishiwa mishahara kutumia mfumo wa HCMIS, watumishi 4454 wamebadilishiwa Muundo, 126,924 kati ya waliokuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara walilipwa na ajira mpya 43,646 zilitolewa. Na kwa takwimu hizo pia Watumishi wa kada mbalimbali wa Halmashauri hiyo walifaidika.

Naibu Waziri aliwahakikishia Viongozi wa Halmashauri hiyo pia, serikali itaendelea kupunguza mapungufu ya wafanyakazi kadri utekelezaji wa mipango ya kibajeti inavyoendelea kutekelezwa na hasa baada ya kupatiwa watumishi zaidi ya 227 Katika bajeti iliyopita ya 2022/2023. 

 Pamoja na hayo Naibu Waziri aliwahakikishia watumishi hapa kuwa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania imeendelea kutengeneza mazingira wezeshi ya Watumishi kufanya kazi na kwamba serikali imeendelea kuweka  mazingira na kuhakikisha kuwa mazingira mazuri ya kufanya kazi. 

Wakati huo huo, Naibu Waziri Kikwete amewataka Maafisa Tawala na Rasilimali Watu kuwahimiza wale ambao hawajachukua haki yao ya Asilimia 5 za michango yao baada ya kuondolewa kazini kwenye zoezi la ulipaji kutokana na michango yao waliyochangia Mifuko ya Jamii waende kuchukua kwani serikali imeendelea kutenga pesa ili kuwalipa stahiki zao. 

Naibu Waziri Kikwete ameeleza kuwa serikali imeendelea kuwalipa na hadi kufika Mwezi Juni 2023, serikali ilipokea Madai 14,147 kati ya watumishi 14,516 waliondolewa na wameshalipa Tshs. Bilioni 42.15 ya madai hayo.

Amesema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano kwa jinsi Dk. Samia Suluhu alivyo na huruma kwa watu wake na kutambua kuwa hata wale waliondolewa nao wana haki yao katika mchango wa Taifa hili la Tanzania.  


Post a Comment

0 Comments

Close Menu