Blog Post

Brigedia Jenerali Kimweri afariki

 Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Mkuu wa Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Brigedia Jenerali Ramadhan Kimweri (mstaafu), amefariki Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu, Brigedia Jenerali Kimweri ambaye alikuwa mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania amepatwa na msiba huo  leo ghafla nyumbani kwake Kibaha mkoani Pwani.

Taarifa zinasema taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Kibaha kwa Mathias, na umma utajulishwa kinachoendelea. 


Post a Comment

0 Comments

Close Menu