Blog Post

NAIBU SPIKA MHE SILLO AITAKA EAC KUTEKELEZA WAJIBU WA KUSHIRIKI KIKAMILIFU SHUGHURI ZA JUMUIA

 Na Mwandishi wetu Arusha


Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Daniel Sillo, ameshiriki katika Mkutano wa 21 wa Maspika wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha.


Mkutano huo ulijadili ajenda mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Michezo ya Mabunge (Inter-Parliamentary Games), michango ya nchi wanachama kwa Jumuiya pamoja na ushiriki wa nchi wanachama katika shughuli mbalimbali za Jumuiya.


Akitoa salamu za utangulizi, Mhe. Sillo alitoa wito kwa nchi wanachama kutekeleza wajibu wao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za Jumuiya ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Aidha, Mhe. Sillo alihakikishia kikao hicho kuwa Tanzania itaendelea kuwa mshirika mwaminifu wa Jumuiya na Bunge lake litatekeleza wajibu wake kuhakikisha shughuli za Jumuiya zinaleta matokeo chanya kwa ustawi wa wananchi wa Afrika Mashariki.


Vilevile, Naibu Spika huyo alieleza kuwa Bunge la Tanzania limejipanga kikamilifu kushiriki Mashindano ya Michezo ya Mabunge yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Desemba, 2026 Jijini Arusha.


Halikadhalika, Mhe. Sillo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Maspika wa nchi wanachama wa EAC katika Mkutano wa 153 wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kuanza Jijini Arusha kuanzia tarehe 05 hadi 09 Oktoba, 2026.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu