Blog Post

RC TANGA MHE BATILDA ASHIRIKI DUA YA KUWAOMBEA MAREHEMU HAFIDH AMEIR NA BI FATMA KARUME

 Na Mwandishi wetu Tanga


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, ameshiriki katika dua maalum ya kuwaombea marehemu *Sheikh Hafidh Ameir* na *Bi. Fatma Karume* , iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa *BAKWATA,* Jukwaa la Wanawake ( *Juwakita)* na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.


Katika dua hiyo *, Mhe. Balozi Dkt. Batilda* amewashukuru viongozi wa BAKWATA, Jukwaa la Wanawake, wanawake kutoka taasisi mbalimbali, watoto wa madrasa pamoja na mayatima kwa kushiriki katika dua na sadaka kwa ajili ya kuwaombea wazee hao waliotangulia mbele ya haki.


Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha utamaduni wa kuwaombea waliotangulia mbele ya haki, kushirikiana katika ibada na kuimarisha mshikamano katika jamii.


 *Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu wetu, awasamehe madhambi yao na awajaalie Pepo. Amina* .

Post a Comment

0 Comments

Close Menu