Blog Post

SERIKALI YAWATOA HOFU WADAU WA POMBE KALI - MHE KAPINGA


Na Omary Mbaraka 


Serikali imekutana na wamiliki wa Viwanda vya kuzalisha pombe kali nchini ikiwa ni hatua ya kuendelea kupambana na bidhaa bandia na duni.


Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga[Mb] akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,  Mhe.Balozi Waziri Salum  kukutana na  kufanya mazungumzo na  wamiliki wa Viwanda vya pombe kali  Agosti 24,2026 Jijini Dar es Salaam, katika kikao kilicholenga kutafuta suluhu ya changamoto hiyo.


Akizungumza katika katika kikao hicho, Mhe.Kapinga amesisitiza umuhimu wa mzalishaji wa pombe kali kuendelea kuzingatia Sheria,taratibu na kanuni za uanzishwaji wa Viwanda hivyo kwa kuzingatia ubora,usafi na afya ya mtumiaji.

Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya jitihada za serikali za kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa rafiki huku Wananchi wakipata bidhaa muhimu na halali kwa bei inayokubalika.


Kikao hicho pia kimeweka mkakati wa pamoja wa kila mzalishaji wa pombe kali kuendelea kutoa Elimu kwa wadau na Wananchi kutofautisha bidhaa bandia na halali.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu