Na Mwandishi wetu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga[Mb] Agosti 24,2026* amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Kenya na Afrika Kusini nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Biashara na Viwanda.
Katika mazungumzo hayo, Kapinga na Balozi wa Kenya, Mhe.Catherine Wahome wamejadili njia za kuboresha mazingira ya biashara na kukuza uchumi wa Mataifa hayo.
Aidha,akiwa na Balozi wa Afrika Kusini, Mhe.Noluthando Mayende-Malepe, wamezungumzia fursa za kuimarisha ushirikiano wa Kiuchumi na uwekezaji kati ya nchi hizo.
Mazungumzo hayo yanaakisi dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendelea kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi kwa maendeleo ya pamoja.




0 Comments