Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea vifaa vya kisasa vya Chumba cha Kanzi Data, vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na miundombinu iliyoboreshwa ya mtandao kutoka Mamlaka ya Taifa ya Nyaraka na Kumbukumbu ya Sultanate ya Oman.
Katika sherehe hiyo Mhe Kikwete ameelezea mchango huo kuwa unalenga kuimarisha usimamizi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali katika mfumo wa kidijitali, kuongeza usalama wa taarifa za Serikali, kuboresha upatikanaji wa nyaraka kwa wakati, kuimarisha uhifadhi wa muda mrefu wa kumbukumbu muhimu za taifa na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za umma na kwa upande mwengine ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano wa kihistoria na ushirikiano imara uliopo kati ya Tanzania na Oman.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali za Tanzania na Oman, akiwemo Balozi wa Sultanate ya Oman nchini Tanzania, Mheshimiwa Said Hilal Al-Shidhani, Balozi Abdallah Kilima kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka.







0 Comments