Na Mwandishi wetu
Kufuatia Ziara ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga[Mb] ,nchini China mwezi Machi 2026 kwa ajili ya kutafuta na kuvutia wawekezaji wa kimkakati katika sekta ya Viwanda,Tanzania imeendelea kuona matokeo ambapo wawekezaji kutoka China wamefika nchini kwa lengo la kuwekeza katika sekta mbalimbali za uzalishaji.
Wawekezaji hao kutoka Jimbo la Guangzhou,wakiwalisha kampuni ya Guangzhou Songesheng Enterprise Management Company Limited,wamefanya Kikao na Mhe.Kapinga Julai 10,2026 kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji nchini.Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Bodi, Bw.Hao Liao ,Mkurugenzi mwendeshaji, Bw.Leon Liao pamoja na Mkurugenzi wa uwekezaji, Bw.Cruld Liao .
Kikao hicho kilikuwa na mafanikio makubwa,kikilenga kujadili fursa za uwekezaji wa Viwanda,kuongeza Biashara kati ya Tanzania na China,uhamishaji wa Teknolojia pamoja na kuimarisha ushirikiano wa Kiuchumi.
Hatua hizi ni sehemu ya Jitihada za serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kukuza uwekezaji,kuongeza thamani ya rasilimali za ndani,kujenga uwezo wa uzalishaji wa ndani na kuunga mkono azma ya Tanzania ya kujenga uchumi shindani wa Viwanda kuelekea kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilion 1 ifikapo mwaka 2050.




0 Comments