Blog Post

UONGOZI WA KATA YA CHANG:OMBE KWA SASA WASHINDWA KUWATETEA WANANCHI KUEPUKA GHARAMA ZA MAISHA

 

Na Ismail Mang'ola 

UONGOZI wa Kata ya Chang'ombe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam umeshindwa kuwatetea Wananchi ambao ndio wapiga kura wao kuepuka gharama za maisha kufuatia kuzibwa njia waliyokuwa wakiitimia tangu miaka mia Kenda iliyopita.


Njia iliyozibwa ni Ile iliyokuwa karakana ya Reli eneo la Mbozi ambayo ilikuwa mahusus kwa ajili ya kupakia nafaka zinazohifadhiwa katika maghala ya Chakula barabara ya Mbozi iliyokuwa upande wa pili wa Toyota barabara ya Nyerere.


Imeelezwa kuwa baada ya kuzibwa njia hiyo na eneo Hilo kupewa mwekezaji, njia hiyo ilikuwa ikutumika kabla hata ya kuanzishwa Viwanda hivyo, na hata baada ya kuanzishwa kwa Viwanda, Bado iliendelea ikutumika.


Lakini kwa sasa Wananchi wanaoishi maeneo ya Chang'ombe, Miburani, wailes, Tandika na maeneo mengine wanaofanya kazi viwandani, wamesema hali hiyo imewaathiri sana hali ambayo wanaona wameongezewa gharama za maisha na Uongozi  wa Kata.


Wamesema kwa sasa wanalazimika kuzunguka umbali mrefu kwa kutumia bodaboda ni zaidi ya Tsh 4000 wakati awali walikuwa wanalipa 1000 Hadi 2000 nyakati za alfajir.


Chanzo hicho kimeendelea kusema kuwa, mzunguko uliopo umekuwa mkubwa kiasi kwamba ili wafanyakazi na wajasiriamali wafike kwenye maeneo ya biashara au kazi.


Wananchi hao wanaiomba Halmashauri ya Manispaa ya a Temeke kupitia ofisini zake za Serikali ya Mtaa wa Toroli na Chang'ombe 'A' kuingilia Kati sakata Hilo ili njia hiyo ifunguliwe ili kupunguza gharama za maisha iliyowakuta wajasiriamali hao kwa kipindi chote baada ya kufungwa njia hiyo.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu