Blog Post

UJIO WA MAGARI YA CHAPA YA JETOUR KUFUNGUA FURSA ZA UCHUMI- KAPINGA





 Na Mwandishi wetu 


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga[Mb], amesema ujio wa magari ya Chapa ya Jetour unakwenda kufungua ukurasa mpya wa fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania kwenye nyanja za mauzo,huduma za kiufundi na teknolojia ya habari na mawasiliano.


Kapinga amebainisha hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa chapa ya Kimataifa ya Magari ya Jetour nchini Tanzania iliyofanyika  Juni 08,2026 Superdome,Jijini Dar es Salaam  ambapo amesema mbali na kukuza  soko la bidaa,ushirikiano huo ni faida kubwa ya uhamasishaji wa teknolojia na maarifa mapya ya kitaalamu nchini kupitia mifumo ya kisasa ya huduma na matengenezo ya magari,mafundi na Wataalamu wazawa watapata mafunzo yakayoinua ujuzi wao,hatua ambayo itaongeza ushindani wa sekta ya magari ya Tanzania na kuinua ubora wa huduma Kimataifa.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu