Blog Post

RAIS DKT SAMIA NA RAIS MHE SHANMUGARATNAM WASHUHUDIA UTIAJI SAINI


Na Mwandishi wetu Dar es salaam 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam wakishuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Singapore kuhusu Uendelezaji Ujuzi na Rasilimali Watu inayokusudia kuimarisha mafunzo ya kitaalamu, Ujenzi wa uwezo na kubadilishana uzoefu katika maendeleo ya Rasilimali Watu. 

Utiaji saini huo umefanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Waziri wa Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje, Familia na Maendeleo ya Jamii Jamhuri ya Singapore, Mhe Zhulkarnain Abdul Rahim, Juni 9, 2026 Ikulu jijini Dar es salaam

Post a Comment

0 Comments

Close Menu