Dar es Salaam . Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) jijini Moscow, Russia, huku akisema heshima hiyo si ya mafanikio yake binafsi bali ni utambuzi wa mchango wa Watanzania wote katika maendeleo ya Taifa na ushirikiano wa kimataifa.