Na Mwandishi wetu Mbeya
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndugu. Ndele Mwaselela Leo tahere 24/05/2026 amekuwa mgeni rasmi katika Kongamano la wanazuoni wa Jumuiya ya Kiislam mkoani Mbeya.
Akizungumza na wanazuoni hao amehimiza Vijana Kulinda Amani na kuwa wazalendo kwa Taifa letu kwani Leo Vijana wameanza kutumika vibaya hasa katika Mitandao ya kijamii.
lakini pia amewataka Vijana hao kutumia fursa za kimazingira katika Kujikwamua kiuchumi kwa Kuthubutu na Kuwa na Bidii ya Kazi na tutumie fursa nyingi tunazo hapa Nchini.
Pia amezidi kuwaasa Vijana kuzidi Kusoma Vitabu ambavyo vitawaweza Kuwajenga kifikra.
na Vyuo vyetu vijenge Vijana ambao watakuwa wazalendo kwa Taifa lao na Waaminifu na kuepukana na Vijana wenye ndimi Mbili. ```"Vijana wenzangu itakuwa furaha yangu kama Elimu zetu tutazitumia vyema na Kuyaishi maadili ya fani zetu na kujiepusha kuwa na Ndimi Mbili tofauti, Mchana hili, Jioni Jingine"```
Aidha MNEC Mwaselela, ametoa nafasi ya Mwanafunzi Mmoja Kulipa ada ya Chuo Kikuu kwa kijana atakayetokana na Jumuiya ya Vijana wanavyuo wa Kiislamu mkoani Mbeya.
Mwisho amemalizia kwa kuwapongeza Vijana hao kwa Kuweza kukaa pamoja na Kuweza kujadiliana mambo yao lakini pia kujadili mstakabali wa Taifa letu, na Kutoa wito kwa wanazuoni wote nchini kulilinda Taifa letu na kumlinda Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani anayemkatisha tamaa rais basi ni anatamani kuliangamiza Taifa letu kwa Ujumla.






0 Comments