Blog Post

KADOGOSA AOMBA SERIKALI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA MAFUTA

Na Omary Mbaraka 


Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa (CCM), ameitaka Serikali kuweka mikakati ya kudumu ya kukabiliana na mgogoro wa mafuta nchini, huku akisema changamoto hiyo si mpya bali imekuwa ikijirudia mara kwa mara.


Mbunge Kadogosa amesema kila mgogoro unapaswa kutazamwa kama fursa ya kujipanga upya kwa mustakabali wa sekta ya nishati. “Crisis inakupa mwanya wa kufikiria… twende zaidi tujiwekee mipango,” amesema.


Kadogosa ameishauri Serikali kuharakisha matumizi ya nishati mbadala kama gesi asilia na umeme, hususan katika usafiri wa umma na magari ya Serikali ili kupunguza utegemezi wa mafuta kutoka nje.


Vilevile, Kadogosa amesema bila mikakati ya muda mrefu, nchi itaendelea kukumbwa na misukosuko ya mara kwa mara ya mafuta, hali inayoweza kuathiri wananchi na uchumi kwa ujumla.


Aidha, amebainisha kuwa historia ya dunia inaonyesha migogoro ya mafuta imekuwa ikijirudia tangu miaka ya 1950 kutokana na matukio mbalimbali ya kimataifa, akisisitiza umuhimu wa maandalizi ya kudumu.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu